Soko la ajira linakabiliwa na mabadiliko makubwa siku zijazo kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, mwenendo wa dijitali, na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
Kwa mujibu wa BBC, hizi ni baadhi ya ajira zinazotegemewa kufanya mapinduzi makubwa katika soko la ajira kwa miaka ijayo;
Mtaalamu wa akili bandia na mtaalam wa kujifunza mashine
Wataalamu wa akili bandia wanatarajiwa kuunda mifumo ya kompyuta inayoweza kufikiria kama watu na kutatua matatizo magumu. Kazi hii pia inalenga zaidi kuwezesha mfumo wa akili wa bandia kuwa na uwezo wa kutatua shida, kujibu maswali na kukamilisha kazi ambazo kawaida hufanywa na wanadamu.
Mtaalamu wa uendelevu wa mazingira
Ukifanya kazi hii utakuwa mshauri ambaye majukumu yake yanabadilika kulingana na shirika unalofanyia kazi. Inahusisha kusimamia miradi ya kupunguza uzalishaji wa gesi inayochafua mazingira, kupunguza matumizi ya nishati au kushiriki katika uundaji wa sera za mazingira katika mipango ya uwekezaji.
Ingawa mtaalamu wa aina hii huwa na masomo yanayohusiana na sayansi ya mazingira, inahitaji ujuzi wa kukusanya na kuchanganua data, kutambua matatizo na kupendekeza suluhisho ambalo linafaa kwa kampuni.
Mchambuzi wa Biashara (Business Intelligence Analyst)
Mchambuzi wa biashara (BI) husoma na kuchambua data ili kusaidia kampuni kufanya maamuzi ya biashara.
Kwa kuchakata kiasi kikubwa cha habari, mchambuzi hutambua hatari zinazoweza kukumba biashara na kupendekeza mabadiliko ili kuboresha ufanisi na tija ya kampuni
Kwa ufupi, mtaalamu huyu husoma michakato ndani ya kampuni, hukagua na kuchanganua data ya mshindani, hutambua fursa, na kupendekeza jinsi ya kushughulikia changamoto za biashara.
Mchambuzi wa usalama wa habari
Mchanganuzi wa usalama wa habari hulinda mifumo, hifadhidata na aina yoyote ya taarifa nyeti dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.
Kutokana na hili, mtaalamu hufanya kazi ya kurekebisha, kufuatilia, kudhibiti mifumo ya ulinzi na kukabiliana na mashambulizi. Wale wanaoanza kazi wanahitaji kuwa na angalau shahada katika sayansi ya kompyuta.
Mwendeshaji wa zana za kilimo
Kazi yake kubwa ni kuendesha mashine za kusaidia shughuli za kilimo, kama vile kulima, kupanda na kuvuna mazao, kulisha mifugo na kuondoa taka zao.
Unaweza pia kufanya kazi kama vile kuweka maganda, kumwagilia kuendesha magari, au zile zinazohusiana na kushughulikia vifaa vinavyotumika baada ya kuvuna