Sekta binafsi Tanzania inavyosaidia kupambana na homa ya kirusi cha Corona

0
42
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu

Katika siku za karibuni kumekuwa na habari nyingi kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa kupambana na kuenea kwa homa ya kirusi cha corona.

Wiki hii serikali ya Tanzania imetangaza mpango kujenga hospitali ya kupambana na magonjwa ya mlipuko kama homa hii ya kirusi cha corona. Hospitali hiyo inayokadiriwa kuwa itagharimu shilingi bilioni 7 za Kitanzania inatarajiwa kumalizika ndani ya miezi sita. 

Mbali na hilo, ni faraja kubwa kuona nchi mbalimbali zinakuja pamoja kuhakikisha maisha yanaendelea na adui huyu wa maradhi haya anashindwa. Kwa mfano Jumuiya ya SADC imezisihi nchi washirika zenye bandari kuweka mkakati kuhakikisha bandari hizo zinaendelea kufanya kazi zikisaidia pia nchi zisizo na bandari kuendelea kupokea mizigo yao kama dawa, vyakula na kadhalika. 

Huku serikali na wadau wengine wakiendelea kufanya kila wawezalo, imekuwa pia jambo jema kuona sekta binafsi nchini Tanzania akishiriki katika vita hii dhidi ya kirusi cha corona. 

Mfano kampuni ya Oryx Gas imetoa gesi ya kupikia yenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa mahospitali na vituo vya afya. Kampuni ya Puma Energy yenyewe imetoa 50,000 kuwezesha gari za kubeba wagonjwa na zile za kubeba madawa.

Mitandao ya simu nayo haiko nyuma. Kampuni kama Tigo Tanzania pamoja na mambo mengine inasaidia wenye biashara ndogo na za kati kuwa na mtandao imara wa intaneti kuendelea kufanya biashara na mawasiliano muhimu yanayohitaji data kama mikutano, kuuza bidhaa, kutangaza bidhaa na kufanya malipo. Hii inasaidia wanaotaka kufanya kazi wakiwa nyumbani kufanya hivyo huku wakifurahia intaneti kutoka Tigo na router ya bure nayo toka Tigo. 

Tuko kwenye changamoto kubwa kama taifa na juhudi za sekta binafsi kama hizi na za ziada zinasaidia sana jamii na serikali yetu katika kupambana na kuvuka msimu huu tukiwa imara. Tuendelee kushirikiana katika vita hii. Siku njema na angavu zinakuja. 

Send this to a friend