Sekta ya mawasiliano ya simu ilivyo na tija kwa Watanzania

0
42

John Hinju, UDBS


Tanzania imepata bahati kubwa kuwa na sekta ya mawasiliano ya simu ambayo imekuwa ikipanuka kwa kasi kubwa siku hadi siku.


Miundombinu ya mfumo wa mawasiliano nchini kama vile mkonga wa taifa na uzinduzi wa mtandao wa 4G umetengeneza fursa nyingi kwa Watanzania. Kuanzia mawakala wa kutuma na kupokea fedha, wahandisi wa mitambo na mafundi mbalimbali, sekta hii imekuwa na faida lukuki kiuchumi kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, sekta hii mpaka sasa imewekeza jumla ya shilingi za Kitanzania trilioni 6. Uwekezaji huu umewezesha kuwepo maendeleo na uboreshaji mkubwa wa miundombinu na ujuzi kwa sekta hii muhimu sana kwenye uchumi wa nchi yoyote ile. Sekta hii ni mtambuka na husaidia sekta na biashara nyingine kukua.

Kampuni kama Tigo kwa mfano imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba inajenga mazingira mazuri kwa biashara ndogo na za kati kukua. Kwa mfano mpango wa Tigo wa “Tigo Business” ni maalumu kwa wafanyabiashara wa ukubwa mbalimbali kuweza kupata huduma zenye gharama nafuu za intaneti na uhifadhi wa data na takwimu za biashara katika mazingira salama zaidi kiteknolojia.


Kupitia kukuza ajira na kuboresha miundombinu, sekta hii imesaidia Tanzania kupata alama bora zaidi katika vigezo vya Benki ya Dunia kwenye mazingira ya kufanya biashara kwani imetoka katika alama 49.7% mwaka 2015 hadi 54.5% mwaka 2020.

Tukielekea mwaka mpya wa 2021, tuendelee kutambua sekta zinaipa nguvu na kasi uchumi wetu ili tuzipe mazingira ya kukua zaidi. Hatuna budi kuendelea kuiunga mkono sekta ya mawasiliano ya simu kwa kuweka sera na mazingira bora yatakayoiwezesha kukua zaidi na sisi kama nchi kuendelea kuvuna faida zake.

Send this to a friend