Sekta ya mawasiliano ya simu ilivyo nguzo muhimu kuleta mabadiliko ya kiuchumi Tanzania

0
35

Dunia inaendelea kushuhudia maabadiliko makubwa ya kiteknolojia sehemu mbali mbali kwa kasi ya ajabu. Sehemu kubwa ya matunda ya teknolojia mfano matumizi ya simu mkononi ambayo yapo sasa, yasingeweza hata kufikirika mwanzoni mwa karne ya 21.

Ukweli usiopingika ni kwamba, kadiri maendeleo ya teknolojia yanavyozidi kupanuka, ndivyo matumizi ya mtandao wa intaneti yatakavyoongezeka. Kwa mfano, takwimu zilizotolewa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo zinaonesha kuwa matumizi ya data yameongezeka toka 46,000GB kwa sekunde mwaka 2017 na yatafikia 150,700 GB kwa sekunde mwaka 2022.

Vijana wanatajwa kuwa kundi lililo katika nafasi ya kunufaika zaidi na maendeleo haya ya kiteknolojia kutokana na uharaka wao katika kuweza kuitumia teknolojia.

Tanzania kama ilivyo nchi nyingine nayo inaendelea kunufaika na maendeleo haya ya kiteknolojia yanayoshamiri kote duniani. Tanzania imeshuhudia mabadiliko makubwa ya kidijitali huku watu wakitumia fursa hiyo kukuza biashara zao na kuendesha maisha.

Kwa mfano, katika robo ya pili ya mwaka huu wa 2020, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuwa matumizi ya jumla ya fedha kwa njia ya simu yameendelea kuongezeka ambapo jumla ya akaunti zilizosajiliwa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu zimeongezeka kutoka milioni 27 mwezi Aprili hadi milioni 29 milioni mwishoni mwa Juni.
Ukuaji huu wa huduma ya fedha kwa njia ya simu umekuwa muhimu sana kwa namna ambavyo watu wanatumia na kuhifadhi fedha zao.

Maendeleo haya yote yanatokana na jitihada zilizofanywa kuwekeza katika sekta hii na wadau mbalimbali. Mfano mzuri ni Tigo Tanzania ambapo huduma ya fedha ya Tigo (Tigo Pesa) imewapatia wateja wake huduma yenye kasi na njia ya kuaminika ya kuweka na kutoa/kutuma fedha, pamoja na faida nyingine lukuki za kuingia katika mfumo rasmi wa kifedha bila urasimu.

Ama kwa hakika, sekta hii ya mawasiliano ya simu Tanzania imeonesha kuwa ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika nchi kupitia teknolojia.

Tukiwa tunafurahia na kutumia matunda ya sekta hii, tuendelee kuunga mkono sekta kwa kuendelea kuwa na sera rafiki na bora ili sekta hii izidi kukua na kuleta tija zaidi kwenye jamii na uchumi wa Tanzania kwa ujumala.

Send this to a friend