Sekta ya mawasiliano ya simu imebadili maisha yetu, tuisaidie ikue zaidi

0
23

Sekta ya mawasiliano ya simu imebadilisha kwwa kiasi kikubwa namna tunaishi maisha yetu. Kampuni mbalimbali za mawasiliano nchini zanatusaidia kuweza kuwasiliana na wapendwa wetu muda wowote, mahali popote.

Baadhi yetu tumefikia hatua ya kuzizoea na kuziona kama sehemu ya maisha yetu huduma zonazotolewa na makampuni haya. Kampuni hizi zimeenda mbali zaidi ya kutusaidia kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki, na kuleta mabadiliko kwenye mifumo ya kibenki, kubadili namna ambavyo tunahifadhi fedha na kulipa ankara zetu.

Kitu kimoja ambacho baadhi yetu tunashindwa kukielewa ni kwamba, baadhi ya makampuni haya yana athari chanya katika mazingira ya kibiashara nchini Tanzania.

Kampuni hizo hizo ambazo zimetuletea huduma ya fedha kwenye simu, zinatafuta namna ya kusaidia kukuza biashara ndogo na za kati (SMEs), ambacho ndizo uti wa mgongo wa uchumi wetu.

SMEs ni muhimu sana katika maendeleo ya kiuchumi nay a kijamii nchini Tanzania kwani huchangia takribani 1/3 ya Pato la Taifa (GDP) na pia inatoa ajira kwa Watanzania zaidi ya milioni 5.2.

Nchi yote kwa ujumla sasa inasukumwa na makampuni ya mawasiliano kuliko kipindi kingine chochote. Kutokana na umuhimu wake, ni vyema mazingira rafiki yakatengenezwa ili kuweza kuiruhusu sekta hiyo kukua maridadi.

Ni lazima tuwe tayari pale sekta inapotaka kubadilika ili kuweza kuendana na mazingira ya wakati huo.

Wataalamu kama vile mashirika ya kimataifa ya kibiashara kwa makampuni ya mawasilino yamehimiza kuimarishwa kwa sekta y a mawasiliano. Kuimarisha huko kuna maanisha kuwa na mashirika machache katika soko ambayo yataweza kutoa huduma kwa kiwango bora zaidi. Wataalami wamehimiza hilo kwani litasaidia kuhakikisha kuwa wateja wote wanapata huduma bora zinazoendana na thamani ya fedha zao.

Kufanikisha uimarishaji wa soko utapelekea pande zote kufaidika, na pia kutaisaidia sekta ya mawasiliano kuweza kutoa huduma bora mwa mwananchi mmoja mmoja, na kwenye biashara. Watanzania wote inatupasa kuamini kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kuruhusu sekta hii kukua.

Send this to a friend