Sendiga aanza na wakwepa kodi mkoani Iringa

0
37

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga ameigaiza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuwasilisha ofisini kwake majina ya wafanyabishara walioshindwa kulipa madeni yao baada ya makubaliano ya kisheria baina ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo.

Aidha, amemuagiza meneja wa TRA mkoa wa Iringa kukutana na wafanyabiashara hao wanaokimbia kulipa madeni yao, huku akisisitiza kuwa hata wafumbia macho waliopewa maagizo ya kisheria kulipa madeni hayo lakini bado wamekuwa wanakaidi agizo hilo.

Amesema akaunti za wafanyabishara wakubwa ambao wanaodaiwa madeni makubwa zilikuwa zimefungwa hapo awali na kufunguliwa kwa mjibu wa sheria na makubaliano na TRA mkoa wa Iringa kulipa madeni hayo ili waendelee na biashara kama iliyokuwa awali.

“Ngoja niwaambie kuwa bila kulipa kodi nchi haiwezi kukuza uchimi wake wala haitaweza kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati kwa kuwa itakuwa inakosa fedha za kuanzisha miradi mikubwa ambayo inafaida kwa serikali,” ameema Sendiga

Ameiagiza TRA kutoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuepusha wafanyabiasha kufunga biashara zao au kushindwa kulipa madeni ya kodi wanayokuwa wanadaiwa.

Nao baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara wamemsihi RC Sendiga kutosikiliza majungu ya baadhi ya wafanyabishara bali ajikite kutatua changamoto walizomueleza kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa huo.

Send this to a friend