Sensa, uchaguzi Kenya na M-Bet vyatajwa kuchelewesha jezi za Simba

0
15

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vunjabei Group Limited, Fred Ngajiro amesema sababu kubwa ya kuchelewa kufika kwa jezi za Simba SC msimu wa 2022/23 ni mkataba mpya wa udhamini wa M-BET kuchelewa kuidhinishwa, hivyo akawa na muda mchache wa kutengeneza.

Akizungumza na E-Fm, mfanyabiashara huyo maarufu kwa jina la Fred Vunjabei amesema mjadala wa mkataba wa TZS bilioni 26 usingeweza kuchukua siku chache, na kwamba waliona heri wajadiliane kwa kina lakini wapate mkataba mzuri.

“Ingekuwa hatujabadilisha mdhamini mpaka leo hii, jezi zingefika mapema, kila mtu angepata jezi na kungekuwa hakuna shida yoyote,” amesema.

Sababu nyingine aliyoitaja ni changamoto za usafirishaji kutokana na usafiri wa ndege pamoja na meli kubeba zaidi mizigo ya sensa, uchaguzi wa Kenya pamoja na kombe la dunia

Vunja bei amewasihi Watanzania kuwa wavumilivu kwa kuwa kila mtu atapata jezi yake na mpaka kufikia Jumatatu ya wiki ijayo hakuna mtu atakaye kosa jezi Dar es Salaam.

Send this to a friend