Sensa ya Makazi kuanza Agosti 30

0
41

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema zoezi la sensa ya majengo nchini litaanza kesho Agosti 30, 2022 hadi Septemba Mosi mwaka huu.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi, na kueleza kuwa zoezi hilo lenye lengo la kukusanya taarifa za majengo yote ya makazi na yasiyo ya makazi litafanyika nchi nzima.

Karani ajiua saa chache kabla ya Sensa, aacha ujumbe

“Litajumuisha kukusanya taarifa za majengo yote ya makazi na yasiyo ya makazi nchi nzima kwa ajili ya kuboresha sera na kupanga mipango ya kimkakati ya kuboresha sera ya nyumba nchini ili kuwa na sera nzuri zaidi ya makazi,” ameeleza Makinda.

Aidha, ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo Agosti 23 mwaka huu hadi kufikia leo Jumatatu Agosti 29, 2022 saa 2 asubuhi, asilimia 93.45 ya kaya zote nchini zimehesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi.

Makinda amesema mafanikio hayo ni baada ya utayari wa wananchi kushiriki katika zoezi hilo.

Send this to a friend