Sera ya usiri ya Tigo na inavyotumia taarifa za wateja

0
46

Kumekuwa na mjadala mkubwa mtandaoni kufuatia kampuni ya mawasiliano ya simu, Tigo Tanzania kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mjalada huo ulijikita katika usalama na usiri wa taarifa za wateja zinazokusanywa na kama kampuni hiyo ilikuwa sahihi kutoa taarifa za siri za watumiaji wake.

Huenda Watanzania walio wengi huwana utaratibu wa kusoma na kufahamu sera za usiri wa kampuni mbalimbali kabla ya kuanza kutumia huduma zake, na baadaye huona kama kampuni husika imekiuka sheria kutoa taarifa zao.

Kupata majibu ya usahihi au la kwa kilichofanya na Tigo Tanzania, tupitia kwa ufupi sera yake ya usiri:

MIC Tanzania Public Limited Company ambayo ndiyo kampuni mama ya Tigo Tanzania yenye dhamana ya kukusanya taarifa binafsi za watumiaji wanaotumia wa tovuti www.tigo.co.tz inaeleza kwamba inatambua na kuhakikisha usalama na usiri wa taarifa za mtumiaji na ina wajibu wa kuweka wazi sera yake ya usiri ambayo inatakiwa kulandana na matakwa ya sera za kidunia za ulinzi wa taarifa na pia ziendane na sheria za Tanzania.

Kupitia tovuti hiyo, Tigo inakusanya taarifa mbalimbali ambazo ni pamoja na ambazo inazitumia katika kutoa huduma, kuuza bidhaa. Taarifa zinazokusanywa ni:

1. Taarifa za usajili: Jina kamili, umri, namba ya simu, barua pepe, anuani, taarifa za malipo, jina la utambulisho na nywila.

2. Taarifa za utumiaji wa tovuti: Mtandao wa simu, mfumo endeshi wa kompyuta yako, kivinjari (browser), tovuti uliyotokea kufikia tovuti ya Tigo, shughuli zako kwenye tovuti pamoja na kurasa utakazozitembelea au manunuzi utakayofana, tarehe na siku uliyotambelea, na huduma ulizotumia kupitia tovuti.

3. Taarifa za eneo ulilopo

4. Taarifa za programu tumishi ya simu kwa kuzingatia tovuti zilizotembelewa na programu zilizopakuliwa kutoka kwenye mtandao wa Tigo.

Kampuni hiyo imesisitiza kwamba haiombi wala kuchakata taarifa binafsi wa watumiaji wenye umri chini ya miaka 18.

Njia zinazotumika kukusanya kukusanya
Tigo hukusanya taarifa kwa njia mbalimbali, ikiwemo mteja kuwapa moja kwa moja, mfano kupitia tovuti, kujisali kupata habari na taarifa za Tigo au kuwasiliana nao kwa sababu mbalimbali kupitia barua pepe, namba ya simu, fax au kwa njia ya maelezo ya kuandika au kufika mwenyewe katika ofisi zao. Pia hupata taarifa kutoka kwa wahusika wengine (third parties) au taarifa za wazi.

Kwanini wanakusanya taarifa
1. Kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na watumiaji wa mtandao huo.
2. Kwa sababu za kibiashara kama vile kutoa ofa, punguzo la bei, bidhaa, matangazo, fursa mbalimbali, kampeni.
3. Kujenga uhusiano na wateja walengwa kama vile wahisani na wadau wengi ikiwemo jamii kwa ujumla.
4. Kwa sababu za kisheria ikiwemo takwa la kisheria la serikali au taasisi ya kiuongozi katika utekelezaji wa majukumu yake au kwa amri ya mahakama au kulinda haki, mali na usalama wa Tigo pamoja na usalama wa wateja, wafanyakazi na umma kwa ujumla.

Hata hivyo, haitakiwi kuuza taarifa hizo kwa wahusika wengine.

Nani mwingine anaziona?
Tigo inaweza kutumia taarifa zako na wahusika wengine wanaotoa huduma kwa Tigo mfano huduma ya uhifadhi taarifa, kutimiza maagizo, huduma kwa wateja au matangazo. Pia inaweza kutumia taarifa zako na taasisi nyingine ya utunzaji wa taarifa hata kama haijaanzishwa nchini lakini kwa kuzingatia takwa la mahakama na kunapokuwepo na amri ya maandishi, au pale sheria inapoitaka.

Taarifa huhifadhiwa kwa muda gani?
Tigo inatunza taarifa hizo kadiri itakavyoona inafaa au hadi pale haja yao itakapokwisha, au kama wanavyotakiwa na sheria.

Send this to a friend