Serikali: Benki ya Deutsche haidhamini bomba la mafuta (EACOP)

0
39

Wizara ya Nishati imekanusha taarifa zilizokuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kujitoa ufadhili kwa Benki ya Deutsche katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Eacop) na kuweka wazi kuwa benki hiyo haipo kwenye orodha za benki zinazotoa fedha kwenye mradi huo.

Taarifa hizo zimekuwa zikidai, benki hiyo imesitisha mpango wa kufadhili dola za Marekani bilioni 3.5 kwa ajili ya kujenga bomba la mafuta lenye urefu zaidi ya kilometa 1,400 kutoka Uganda hadi Tanzania kutokana na wanaharakati wa mazingira kusema, mradi huo utaondoa familia nyingi na kuleta changamoto kwenye hifadhi za asili.

Viwango vipya vya gharama za kuvuka Daraja la Nyerere

Mratibu wa mradi wa bomba hilo kutoka Wizara ya Nishati Tanzania, Kisamarwa Nyangau amesema tafiti mbalimbali zimefanyika na kuweka mikakati ya kuhakikisha mradi huo hauathiri mazingira kama ambavyo inadaiwa.

“Mradi wa EACOP unaandamwa sana kwasababu kwa sasa uko juu katika kutafuta fedha kwenye soko la dunia, wanaotoa fedha nao walifanya utafiti kujiridhisha kama mradi huu unaweza kukopesheka na wakaridhika,” amesema Nyangau.

Send this to a friend