Serikali imesema hakuna mwanafunzi ambaye amepelekwa kwenye vyuo vya kati bila yeye mwenyewe kupenda, bali wanafunzi wenyewe walifanya machaguo hayo ambayo yalionekana kwenye mfumo.
Amebainisha hayo Naibu Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI, David Silinde alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu aliyehoji sababu za wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na kupata daraja la kwanza na la pili kisha kupelekwa kwenye vyuo vya kati bila wao kupenda.
Serikali: Hatutazuia safari za usiku za mabasi ya ‘hakuna kulala’
Aidha, amesema kuna makosa ambayo yalifanyika kwa wanafunzi wenyewe ambao baadhi yao walijaza kupelekwa katika vyuo vya ufundi kwenye chaguo la kwanza.
“Kuna makosa ambayo yalikuwa yamefanyika kwa watoto wenyewe ambao wengine walijaza chaguo la kwanza kwenda vyuo vya ufundi halafu wakawa wamefaulu, baadaye wakawa wanataka kubadilisha kwenda hatua ya pili [kidato cha tano],”amesema.