Serikali: Hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya gharama za umeme

0
40

Serikali imesema hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya bei kwa wananchi ambao tayari wamelipia kiasi cha TZS 27,00 kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Nishati, Stepehen Byabato bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Issa Mtemvu lililouliza kuhusu Serikali kutoa maelezo juu ya wananchi waliolipia TZS 27,000 lakini bado hawajaunganishiwa umeme.

“Agizo kwa TANESCO kwa ambao tayari walishalipa ni kwamba, hakutakuwa na mabadiliko ya bei, yule ambaye alishalipia gharama ataunganishiwa umeme kwa gharama hiyo hiyo. Nasisitiza kwamba, yeyote atakayeambiwa ulilipa TZS 27,000 lakini sasa unatakiwa kulipa zaidi, tupatieni taarifa ili tufanye ufuatialiaji na kuwajibishana katika eneo hilo,” amesema Naibu Waziri.

Ujenzi wa Mwendokasi Gongolamboto kuanza

Aidha, amebainisha kuwa TANESCO ina idadi kubwa ya wateja ambao tayari wamelipia gharama za umeme hivyo wategemee kuunganishiwa umeme kwa wakati kwa sababu Serikali ya awamu ya sita imewezesha pesa za kutosha kuweza kupeleka umeme kwa wananchi.

Send this to a friend