Serikali kuangalia uwezekano kutoa mikopo kwa wanafunzi wa diploma na cheti

0
14

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaangalia uwezekano uliopo ili kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (ZAHLIFE) Ikulu Chamwino jijijni Dodoma ambapo amesema kwa kazi zinazofanyika nchini na hali ya bajeti, suala la mikopo kwa ngazi hizo litaingizwa kwenye mpango wa Serikali ili liweze kutafutiwa ufumbuzi.

Hata hivyo Rais Samia amewasisitiza wanufaika wa mikopo inayotolewa kurudisha mikopo hiyo mara baada ya kuhitimu masomo yao na kupata ajira ili kuwanufaisha wanafunzi wengine wenye uhitaji.

Aidha, ameiagiza Wizara ya Elimu chini yake Waziri Adolf Mkenda kuangalia na kuipitia upya mitaala inayotumika kufundishia nchini ili iweze kuwaandaa vijana kujitegemea mara baada ya kuhitimu masomo yao.

TEMESA yataka nauli za vivuko zipandishwe

“Kwenye mitaala yetu tulibeba mambo mengi chungu nzima. Tukafundisha watoto kuanzia la kwanza mpaka vyuoni, lakini bado kundi kubwa la vijana hatukuwatayarisha kwamba wanapotoka vyuoni waweze kujiajiri, hatukufanya hivyo,” amesema Rais Samia.

Kwa aupande wake Waziri wa Elimu, Adolf Mkenda amesema Wizara imeunda kamati ili kuangalia vigezo vinavyoweza kutumika wakati wa kutoa mikopo ili iweze kuwafikia walengwa zaidi wa mikopo hiyo.

Send this to a friend