Serikali kuanzisha bima ya safari kwa raia wa kigeni wanaoingia nchini

0
178

Serikali imetangaza kuanzisha bima ya safari kwa raia wa kigeni wanaoingia Tanzania Bara itakayogharimu Dola za Marekani 44 [TZS 116,100].

Leongo la bima hiyo ni kwa ajili ya matibabu ya dharura kwa wageni wanapokuwa nchini, kupotea kwa mizigo, huduma za uokoaji, na kurudishwa kwa mgeni nchini kwake iwapo itatokea dharura.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha imesema ukataji wa bima kwa raia wa kigeni watakaoingia nchini utaanza rasmi baada ya kanuni za usimamizi wa bima ya safari kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali ambapo umma utajulishwa baada ya hatua hiyo kukamilika.

Send this to a friend