Serikali kuchukua hatua video ya wanafunzi inayosambaa mitandaoni

0
27

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kufuatilia utovu wa nidhamu uliofanywa na baadhi wa wanafunzi wa shule za Wilaya ya Kisarawe wakati wa mahafali ya kidato cha nne.

Akizungumza katika mahafali ya shule za Kiislamu za Ilala yaliyofanyika katika Uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam amesema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote walioruhusu vitendo hivyo kufanywa na wafunzi na kuongeza kuwa video hizo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilishtua Serikali, viongozi wa dini na jamii kwa ujumla.

“Ninalaani vikali sana wale walioruhusu ule mchezo wa shule hizo pale Kisarawe na picha zikapigwa, haiwezekani walimu hawakujua, hairuhusiwi na tunaahidi kwamba tutachukua hatua zaidi,” amesema.

Ameongeza kuwa wazazi wamewapa shule jukumu la kuwalea watoto wao katika misingi mizuri ikiwemo kuwakuza kimaadili kwa kuwa wao wanakaa nao muda mrefu.

Send this to a friend