Serikali kudhibiti utozaji nauli za teksi

0
87

Wakala wa Vipimo [WMA] umesema inakwenda kuchukua hatua na kufanya uhakiki wa vipimo halali kwa kampuni za simu, kutokana na madai ya muda wa mrefu kutoka kwa jamii kutoridhishwa na muda wa maongezi na matumizi kutolingana na gharama wanazolipia.

Akizungumza Ofisa Vipimo Mkuu kutoka WMA, Gaspal Matiku amesema taasisi hiyo imeanza mchakato wa kuzifikia kampuni za simu ili kupata vipimo halisi katika mita za maji, umeme, pampu za mafuta na vyombo vya usafiri hususani usafairi wa teksi kwa kuwa umbali wanaosafiri wateja haulingani na gharama zinazotozwa.

“Tunatarajia kuingia katika eneo la mawasiliano ambapo tutadhibiti matumizi ya muda wa maongezi na mteja atalipa stahiki na huduma anayopata, hii biashara imekuwa huria, tutahakikisha tunatumia sheria kudhibiti mitandao ya kijamii iendane na thamani halisi ya matumizi na fedha anayolipwa mtu,” amesema.

Aidha, amesema ili kuleta usawa katika biashara ya usafirishaji, kutakuwa na ufungaji wa vifaa maalum katika vyombo vya usafiri ikiwemo teksi, ambapo mteja atalipa nauli sahihi kulingana na umbali wa safari.

Ameeleza kuwa katika sekta hiyo ya usafiri vipimo hivyo vitahusisha upimaji upepo katika matairi ili kuimarisha usalama wa safari kwa abiria na kukidhi viwango.