Serikali kufanya utafiti kuibaini kiasi cha dhahabu kilichopo nchini

0
43

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeleza utafiti zaidi katika maeneo ya uchimbaji madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichopo nchini, hatua ambayo itawawezesha kuwapanga vizuri wachimbaji wadogo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani Ruangwa mkoani Lindi, amesema mkoa huo una fursa nyingi za uchumi ikiwemo madini, kilimo, uvuvi, gesi, na utalii na kwamba tayari kuna wawekezaji wanne wa madini ambao watafika Ruangwa kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta hiyo ili kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huo.

“Moja kati ya mambo tutakayovifanya ni kuendeleza utafiti zaidi katika maeneo ya madini ili tuweze kujua kiasi cha dhahabu tulichonacho na tuweze kuwaweka vizuri wachimbaji wadogo wachimbe kitaalamu na kuweza kunyanyua kipato na maisha yao,” amesema.

Mbali na hayo, amesema Serikali imedhamiria kufungua mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kwa mwaka huu wa Fedha 2023/24 takribani bilioni 77 zimeelekezwa katika wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Send this to a friend