Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema katika bajeti ya mwaka 2023/2024 Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga nyumba 4,040 za maafisa ugani ili waishi karibu na maeneo ya kazi.
Hayo yamejiri baada ya Serikali kugundua kwamba asilimia 80 ya maafisa ugani nchini hawaishi mashambani wanaishi mijini baada ya kuwafuatilia kupitia GPS za pikipiki walizopewa.
“Tumegundua asilimia 80 ya maafisa ugani hawaishi mashambani, wako mijini, tutatenga bajeti ya kujenga nyumba za maafisa ugani kwenye kata, ahamie kijijini alipo mkulima, kule kuna ward resource centers [vituo vya rasilimali za kata] zilitelekezwa, tutajenga nyumba,” amesema.