Serikali kuongeza kima cha chini cha mishahara Sekta binafsi

0
41

Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako imesema iko katika hatua za mwisho za kutangaza ongezeko la kima cha chini cha mishahara katika sekta binafsi.

Ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akifungua mkutano mkuu wa 63 wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) pamoja na kongamano la waajiri.

Aidha, amesema Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inakua na kustawi.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na waajiri wote hususani wa sekta binafsi katika kuibua fursa za maendeleo, kujadili changamoto mbalimbali pamoja na kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.

Send this to a friend