Serikali kupitia kodi kwenye taasisi za kidini

0
38

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inafanya tathmini kwenye taasisi za kidini ili kubaini zinazofanya biashara elimu na afya na zile zinazotoa huduma ili kuweza kuangalia suala la kodi.

Rais ametoa ahadi hiyo mbele ya viongozi wa dini wakati akihutubia kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 na Kongamano la Wachungaji na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania katika Chuo Kikuu cha St. John’s Jijini, Dodoma.

Katika hotuba ya viongozi hao wameomba serikali kuangalia upya suala la kodi kwani taasisi zao hazifanyi biashara lakini zimekuwa zikilipa kodi sawa na taasisi zinazofanya biashara na kupata faida.

“Kuhusu kodi, niliagiza  taasisi za dini zinatoa huduma za elimu na afya, nataka nipige mstari neno huduma na sio zinazofanya biashara ya elimu na afya, kodi ziangaliwe kwa sababu malalamiko katika suala hili yalikuja siku nyingi, tukaangalia tukakuta viwango vinavyotozwa na taasisi za dini kwenye afya na elimu havipishani na viwango vinavyotozwa na watoa huduma sekta binafsi,” amesema Rais Samia akijibu changamoto hiyo.

Amesema kwa zile zinazotoa huduma wataangalia kodi, lakini zile zinazofanya biashara, ni lazima zilipe kodi.

Rais ametumiwa jukwaa hilo kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuwainua Wanawake kijamii, kiuchumi, kisiasa pamoja na kupambana na ukatili dhidi yao.

Amesema Serikali inafanya hivyo sio kwasababu kuwa yeye ni Rais Mwanamke, bali kwa kuwa mwanamke ana haki sawa kama mwanaume isipokuwa kinachowatofautisha ni makuzi na imani zao.

Send this to a friend