Serikali kupitia upya tozo za stempu za kielektroniki

0
11

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepanga kuangalia upya tozo za stempu za kielektroniki (ETS) ambazo kwa miaka mitatu iliyopita sekta ya viwanda imekuwa ikilalamika kuwa tozo hizi zimekuwa kubwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara, Lawrence Mafuru alipokuwa katika ziara ya kutembelea viwanda vya kutengeneza bia vya Tanzania Breweries Ltd na Serengeti Breweries Ltd jijini Dar es Salaam.

“Kuna haja ya Serikali kusikiliza hoja hii, haiwezekani kwamba kuna kitu ambacho wenzetu wanakiona na sisi hatukioni. Kwa mrejesho ambao tumeupata na sisi tumejionea mfumo unavyofanya kazi, lakini pia tumepata fursa ya kuona mfumo mwingine ambao unafanya kazi sambamba na mfumo unaolalamikiwa,” amesema Mafuru.

Aidha, Mafuru ameongeza kuwa ili kuongeza uwekezaji nchini inapaswa kuwawekea mazingira rafiki ya kuwa na uhakika kama mitaji yao iliyopo hapa Tanzania italindwa ili waweze kuleta mitaji mingine.

Send this to a friend