Serikali kurahisisha gharama za ununuzi wa gesi

0
46

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali inakamilisha utaratibu wa kumwezesha mteja kununua gesi kwa bei ndogo kulingana na mahitaji yake.

Waziri huyo amesema wananchi wengi wanashindwa kumudu kutokana na gharama kubwa zilizopo, hivyo mchakato wa kuzipunguza unaelekea mwishoni ili kutoa ahueni kwa wananchi.

Matibabu ya fistula kutolewa katika hospitali zote za mikoa

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Mwananchi siku chache baada ya Waziri huyo kuhitimisha ziara yake aliyoifanya katika mikoa ya Mara, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Simiyu, Geita na Kagera.

“Moja ya vikwazo kwa Watanzania kutumia gesi ni kwamba lazima uwe na fedha nyingi kwa mkupuo. Teknolojia inayoruhusu mtu kununua gesi ya Shilingi 500 au 1,000 ipo. Baada ya muda tutaileta sokoni ili watu waanze kununua gesi kama wanavyonunua kopo la mkaa au fungu la kuni,” amesema.

Makamba amebainisha kuwa, kiuhalisia bei ya gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni, lakini wananchi wamezoea kununua kuni na mkaa katika vipande vidogovidogo na ndio maana haionekani kuwaumiza wengi, hivyo gesi inahitaji ubunifu wa kibiashara ili kuendana na uwezo na mahitaji ya Watanzania.

 

Send this to a friend