Serikali kurejesha matumizi ya kadi kwa abiria mabasi ya Mwendokasi

0
59

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameagiza kuanzia Julai Mosi mwaka huu, kuanza uhakiki wa tiketi za kielektroniki katika usafiri wa mabasi yaendayo kwa haraka kwa kutumia mfumo wa posi ili kudhibiti upotevu wa mapato

Amesema kuwa utekelezaji wa hilo ni hatua za awali wakati unasubiriwa mfumo mkubwa utakaohuisha matumizi ya kadi na mageti ambao ndio utakaokuwa ni suluhu ya kudumu.

Waziri Ummy ametaka uhakiki huo wa kutumia posi kuanza haraka wakati mfumo mkubwa unaotarajiwa kutekelezwa Novemba mwaka huu, unasubiriwa ili kuepuka udanganyifu, wizi na upotevu wa mapato.

“Nataka mapema tuwe tumekomesha utoaji wa tiketi zisizohakikiwa, hapa tunaruhusu wizi kufanywa watu wanakuwa na vitabu vyao vya tiketi, Rais Samia na Waziri Mkuu waliyasema haya,” amesema Waziri Ummy

Ameendelea kusema kuwa matumizi ya tiketi hizo kunapelekea kujitokeza kwa udanganyifu na wizi wa mapato kutokana na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuingiza sokoni tiketi zao na kusisitiza kuwa lazima kuwepo kwa utaratibu unaohakikisha tiketi zinatolewa moja kwa moja katika mashine na kumfikia abiria wakati huo.

Send this to a friend