Serikali kutoa mikopo kwa baadhi ya fani vyuo vya kati

0
38

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amependekeza kuanzishwa kwa programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu.

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 bungeni jijini Dodoma Dkt. Mwigulu amesema mapendekezo hayo ni kufuatia mabadiliko ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, toleo la Mwaka 2023 na mabadiliko ya mitaala yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ambapo Serikali inalenga kutoa elimu ya amali kwa ngazi zote itakayomuwezesha kijana wa kitanzania kujiajiri au kuajiriwa.

“Napendekeza kuanzisha programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu. Hatua hii itaanza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2023/24,” amesema.

“Nilisema hotuba hii imebeba hotuba ya Mama namna anavyotaka kuwasaidia watoto wa maskini. Pochi ya Mama imefunguka. Mama yuko kazini,” amesema Waziri Mwigulu.

Hatua hiyo imekuja meizi michache baada ya Rais kuongeza kiwango cha posho ya kujikimu maarufu kama ‘boom’kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka TZS 8,500 hadi TZS 10,000 kwa siku.

Send this to a friend