Serikali kutoa Mwongozo wa Maadili ya Kitanzania

0
15

Serikali imesema imekamilisha uchapishaji wa kitabu cha mwongozo wa maadili, na sasa inaendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu maadili ya Mtanzania.

Akizungumza Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul wakati akizindua msimu wa 8 wa Tamasha la Majimaji Selebuka wilayani Songea mkoani Ruvuma, ameeleza kuwa ukusanyaji wa maoni utakapokamilika, Serikali itakuja na mwongozo wa maadili ya Taifa ili kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa katika maadili sahihi.

“Mhe Rais hafurahishwi na mmomonyoko wa maadili katika Taifa letu, na hivyo tuna kazi ya kuwalea vijana wetu kwa kupitia matamasha kama haya ya utamaduni kujua tulipotoka na tulipo, na pia kujua mila na destruri zetu zile zilizo nzuri,” amesema Naibu Waziri Gekul.

Kwa upande wake Mbunge wa Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema licha ya tamasha hilo kutoa burudani kwa wananchi, pia ni sehemu ambayo watu wanaweza kujifunza tamaduni pamoja na wajasiriamali kupata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao.

Send this to a friend