Serikali kutunga sheria kulinda faragha na taarifa za wananchi

0
46

Serikali inakusudia kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi kwa lengo la kuhakikisha taarifa binafsi na faragha  za watu zinalindwa.

Hayo yameelezwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia  ya Habari ambayo imewataka wananchi  kutumia vyema huduma za mawasiliano ya mitandao ya kijamii.

Waizara imewataka wananchi kutumia mitandao hiyo kwa shughuli za kijamii na kiuchumi badala ya  kusambaza taarifa za uongo na kupotosha umma.

Aidha, wizara imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa  inakusudia kuandaa sheria maalumu ya kuwa na laini moja ya simu kwa kila kampuni ya simu ikiwa ni njia ya kulinda faragha za watu inayolenga uhalifu mitandaoni.

Wizara imesema masuala ya usajili wa laini  za simu yameanishwa katika kanuni za usajili wa laini za simu za mwaka 2020 ambazo zinaeleza idadi ya laini zinazoweza kumilikiwa pamoja na utaratibu wa kusajili laini hizo.

Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti uhalifu mitandaoni.

Send this to a friend