Serikali kuwachukulia hatua walimu watoro

0
43

Serikali wilayani Mbeya imewatahadharisha walimu wanaotoroka kazini na kwenda kufanya shughuli zao kwamba watachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa kuwa wanakiuka mikataba ya kazi zao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Vincent Mbua alipokuwa akizindua mkakati wa uimarishaji wa ujifunzaji ngazi ya elimu ya Msingi na Sekondari ulioandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amesema utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini asilimia kubwa ya walimu wamekuwa wakifika shuleni asubuhi na kujiandikisha kwenye vitabu kisha huondoka kwenda kufanya shughuli zao bila kufuata utaratibu, jambo ambalo linazorotesha elimu na wanafunzi kukosa baadhi ya vipindi.

“Utafiti huo ambao tuliufanya kwa siri ulionesha kuwa walimu hawa wakiondoka asubuhi huwa wanarudi tena jioni na kutia saini kuashiria kwamba walikuwepo kazini. Jambo hili nawahakikishia kwamba tutaanza kuwachukulia hatua za kiutumishi,” amesema Mbua.

Send this to a friend