Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema italipa gharama zote safari na kujikimu kwa mashabaiki wa Yanga kwenda Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Hatua hiyo imekuja baada ya Yanga kupeleka ombi maalumu kwa Waziri Dkt. Damas Ndumbaro la kusafirisha mashabiki kwa basi.
“Hapo mwanzo tulitangaza watu watakaosafiri walipaswa kuwa na shilingi 600,000, tulipata watu 30. Niwahakikishie baada ya wizara kukubali kusafirisha wanachama na mashabiki wetu, zile 600,000 zitarudishwa kwa wenyewe,” amesema Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said.
Mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utachezwa Aprili 5 katika Uwanja wa Loftus Versfeld, jijini Pretoria nchini Afrika Kusini, ambapo mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu.