
Boeing and Ethiopian Airlines announced today an agreement for the East African airline to purchase eight 777-9 passenger airplanes and the potential for up to 12 additional jets. (Image: Boeing)
Serikali imetangaza kuwa raia 42 wa Kitanzania waliokuwa wamekwama nchini Israel kutokana na mgogoro unaoendelea, wanatarajiwa kuwasili nchini leo, Juni 25, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Watanzania hao watarejea kwa makundi mawili tofauti kupitia ndege za Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines.
Kundi la kwanza linatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, majira ya saa 6:55 mchana.
Kundi la pili litatua moja kwa moja katika Uwanja wa Ndege wa JNIA kutoka Addis Ababa majira ya saa 11:55 jioni siku hiyo hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa urejeshaji wa Watanzania hao umetokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, aliyetoa maelekezo ya kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuhakikisha usalama wa raia wa Tanzania walioko nje ya nchi.
Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Israel imeongoza juhudi za kuwaokoa na kuwarudisha nyumbani.







