Serikali kuweka utaratibu wa wananchi kukopeshwa smartphones

0
34

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali ina mpango wa kutafuta njia ili kumwezesha Mtanzania wa kawaida kumudu gharama za kununua simu janja (Smartphone) kwa kukopewa mkopo na kurejesha kidogokidogo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mnara wa mawasiliano ya simu katika kijiji cha Kinenulo mkoani Njombe uliojengwa kupitia ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF ), waziri amebainisha kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anaunganishwa na huduma ya mawasiliano.

Aidha, amesema tayari wameanza mchakato kwa kufanya mazungumzo na kampuni mbalimbali za simu kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.

Nigeria kuzindua roboti wa Kiafrika anayezungumza Kiswahili

“Na mimi kwa sababu naipenda kazi yangu nimeshaanza kuhangaika tumebanana na makampuni ya simu tunatafuta utaratibu ambao makampuni ya simu na watoa huduma wengine wataleta simu walau iwe ni kwa mkopo mtu alipe taratibu lakini aipate huduma aanze kutumia.

Mtu wa kawaida kuchukua laki tatu ukaenda kununua simu kidogo ngumu lakini tukimwambia weka Elfu 30 upewe simu ya laki tatu alafu utakuwa unakatwa kidogo kidogo hata kama ni kwa mwaka mzima, huduma unapata, umepata kwa bei ndogo na maisha yanaendelea na maagizo hayo ameyatoa Rais Samia,” ameeleza.

Send this to a friend