Serikali: Kuwekeza kwenye vitu ndio kunawezesha maendeleo ya watu

0
42

Serikali imesema kuwa nchi haiwezi kupata maendeleo ya watu bila kuwekeza kwenye vitu, ndiyo maana awamu ya tano imewekeza kwenye vitu ikiamini vitachagiza maendeleo ya watu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amabaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ambapo ameongeza kuwa kuwa kila sekta ambayo Serikali imewekeza inachangia katika kuleta mageuzi kwa wananchi wa kawaida kwa kutoa ajira mfano sekta ya viwanda ambayo amesema imeajiri watu zaidi ya 200,000.

Dkt. Abbasi amesema uchumi wa Tanzania haujawahi kushuka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita ikiwa ni malengo ya nchi iliyojiwekea kwa muda wa kati na mrefu kwamba uchumi wake ukue kwa zaidi ya asilimia 6.

“Katika miaka mitano kazi kubwa imefanyika na sisi kama serikali tumetimiza wajibu wetu, tunaiona nchi yetu inaendelea kupata maendeleo kwa kasi. Uchumi wetu haujawahi kushuka kwa miaka 10 iliyopita, kwa takwimu za Benki ya Dunia (WB) kama hali ya ukuaji wa uchumi ikiendelea hivi huenda mwaka 2021 au 2022 tukaingia kwenye uchumi wa kati lakini ule wa chini kidogo,” amesema Dkt. Abbasi.

Akizungumzia kuhusu mradi wa bomba la mafuta, amesema kuwa mradi huo haujafa, ni wazo ambalo viongozi wamelipigania hivyo ni lazima litekelezeke. Kwa Tanzania hatua nyingi zimeshakamilika na kwenye mwezi Julai, 2020 Tenda zitaanza kutangazwa.

Send this to a friend