Serikali kuyafungulia magazeti ya Mawio, TanzaniaDaima, Mseto na Mwanahalisi

0
29

Serikali imeeleza kuwa inaendelea na mchakato wa kuyafungilia magazeti manne yaliyofungiwa ambayo ni Mseto, Mwanahalisi, Mawio na TanzaniaDaima ili yaweze kuendelea kuuhabarisha umma.

Hayo yamedokezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mkoani Morogoro, muda mfupi baada ya Makamu Mwenyekiti wa TEF kulalamikia kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari.

“Hatua kadhaa zinaendelea ndani ya serikali ili na wao waweze kurejea kwenye uandishi wao. Na kwakuwa yalifungiwa kwa mujibu wa sheria, sheria zilezile zitafuata utaratibu wake kwa maelekezo ya Mhe. Rais ili na wao waweze kukamilisha au kuondokana na makosa hayo ili viweze kufanya kazi,” ameeleza Waziri Mkuu.

Kuhusu uwepo wa sheria zinazodaiwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ameagiza TEF kuorodhesha vipengele vya sheria hizo, vipelekwe wizarani, wiara iandae muswada kwenda bungeni, ili viweze kufanyiwa marekebisho mwishoni mwa bunge la bajeti.

Hata hivyo ametoa raia kwao kuwa mabadiliko wanayoyataka lazima yalinde tunu za Taifa, amani, muungano, mapinduzi ya Zanzibar. Pia yalenge kuwaweka watu pamoja na kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana.

Awali akitoa hotuba yake, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alisema jukwaa hilo linalaani vitendo vya baadhi ya maofisa wa polisi na watumishi wa serikali kuwapiga, kuwadhalilisha na kuharibu vifaa vya kazi vya waandishi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Send this to a friend