Serikali kuzifuta baadhi ya kampuni binafsi za ulinzi

0
62

Jeshi la Polisi limesema kuwa litayafuta makampuni binafsi ya ulinzi yasiyofuata sheria za nchi pamoja na masharti ya vibali vyao.

Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa linafanya uhakiki wa kampuni hizo ili kubaini kampuni zilizo hai na zinazotekeleza maelekeo kulingana na vibali vilivyotolewa na jeshi hilo vya kuanzisha kampuni mpya za ulinzi.

Wakurugenzi au wamiliki wa kampuni hizo wametakiwa kupeleka vibali vyao jeshi la polisi kwa ajili ya uhakiki kuanzia Oktoba 1 hadi 31, 2021.

Baada ya uhakiki huo, ukaguzi utafanyika na hatua stahiki zitachukuliwa kwa kampuni zitakazobainika kutofuata sheria na kukiuka taratibu ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

Send this to a friend