Serikali: Marufuku chekechea hadi darasa la nne kukaa bweni

0
43

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi darasa la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Akitoa taarifa hiyo, Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023 ikiwa ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Novemba mwaka 2020.

Bashe aagiza Dkt. Mshindo Msola akamatwe

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule kupokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi darasa la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao, kujenga maadili na kushikamana na familia na jamii zao.

Aidha, wizara imesema pia hairuhusiwi kwa shule yoyote kuwa na makambi ya kitaaluma, ambapo imezielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Send this to a friend