Serikali: Marufuku taasisi kufungia biashara

0
40

Serikali imependekeza kuanzia Julai 1, mwaka huu iwe ni marufuku kwa taasisi yoyote ya Serikali kufunga biashara, ofisi ama maeneo yoyote ya uzalishaji kwa kigezo cha kukiuka taratibu mbalimbali.

Akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imependekeza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zirekebishwe ili kumchukulia hatua mwenye biashara kwa makosa ya biashara na siyo kuifunga biashara yenyewe.

TMB: Marufuku kutumia magogo buchani

Aidha, katika bajeti hiyo Dkt. Nchemba ametoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho katika sheria ya ushuru wa barabara na mafuta kwa kuongeza TZS 100 kwa kila lita ya mafuta ya petrol na dizeli ambapo fedha zitakazokusanywa zitatumika katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, iIi kupata vyanzo vya uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mbali na hayo, amependekeza kuongeza ushuru kwenye vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy drink) zinazoagizwa kutoka nje kutoka shilingi 589.05 kwa lita hadi shilingi 600 kwa lita, lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani na kuvifanya viwe shindani, amabapo hatua hiyo inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 36.9.

Send this to a friend