Serikali: Megawati 190 za umeme hazipatikani kutokana na upungufu wa maji

0
49

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema changamoto iliyopo ya kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo nchini ni kutokana na upungufu wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme hasa kwenye maji.

Akizungumza Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati alipoombwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kufafanua tatizo la ukosefu wa umeme katika maeneo mengi nchini, amesema takribani megawati 190 hazipatikani kama ilivyotarajiwa kwa sababu ya upungufu wa maji na kupelekea kukatika kwa umeme nchini.

Bei ya mafuta yashuka, hizi ni bei kwa mikoa yote nchini

“Serikali imetenga bilioni 500 kwa ajili ya kuimarisha gridi, lakini bilioni 300 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mingine isiyokuwa ya gridi, kuhakikisha kwamba umeme haukatiki katiki,” amesema.

Aidha, Naibu Waziri amesema Serikali inahakikisha kabla ya mwezi Desemba kumalizika mradi wa Kinyerezi 1 Extension utakaotoa megawati 185 unakamilika ili kuondoa matatizo ya kukatika kwa umeme.

Send this to a friend