Serikali: Mjamzito akifariki kwa uzembe Mganga Mkuu wa Mkoa, Wilaya ni watuhumiwa

0
39

Serikali imesema matatizo yanapotokea katika sekta ya afya ikiwemo daktari kufanya uzembe, watu wengine watakaokuwa watuhumiwa ni waganga wakuu wa wilaya na mikoa kwa kushindwa kuona na kutatua changamoto kabla hazijatokea.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

“Tukija kwenye mkoa wako tukakuta uzembe umetokea mama mjamzito amefariki na Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni mtuhumiwa mpaka vyombo vitakapo chunguza, tukikuta mama, mtoto au mtu yoyote amepata shida alafu mganga mkuu wa mkoa, wilaya na wewe unashangaa inabidi ujitafakari,” amesema.

Utafiti: Dar yaongoza kwa wanawake kuharibikiwa mimba

Aidha, amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma katika hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya na kuhakikisha wanawajengea uwezo watumishi ili kuepuka changamoto na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa afya nchini.

Send this to a friend