Serikali: Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi nyingine

0
21

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kwa mujibu wa sheria za nchi, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi lolote la nchi nyingine kwani ni kosa kisheria.

Ameyasema hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax wakati akitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kuhusu kifo cha Mtanzania Nemes Tarimo aliyeuawa wakati akishiriki vita nchini Ukraine.

“Nikumbushe kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi lolote la nchi nyingine, ukifanya hivyo ni kuvunja sheria na taratibu za nchi yako. Unaruhusiwa tu kuandikishwa na jeshi la nchi yetu kwa taratibu zilizowekwa, katiba ziko wazi kwamba Mtanzania hawezi kutumikia jeshi la nchi nyingine,” amesisitiza.

Masharti manne yaliyopunguzwa Bima ya Afya kwa Wote

Aidha, amesema Wizara imeendelea kuwasiliana na Serikali ya Urusi kuhakikisha mwili wa Mtanzania Nemes unafikishwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake, na kwamba mwili huo umeondoka nchini Urusi asubuhi Januari 24, 2023 hivyo unategemewa kuwasili nchini wakati wowote.

Hata hivyo, Dkt. Stergomena ametoa rai kwa Watanzania wote walioko nje ya nchi na ndani kuwa wana wajibu wa kutimiza matakwa ya kisheria ya nchi bila kujali mahali walipo.

Send this to a friend