Serikali: Pikipiki zimeua watu 1,113 mwaka 2022-2024

0
33

Serikali imesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2024, jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababishwa na pikipiki nchini.

Akizungumza bungeni leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amesema madereva wa pikipiki waliopata ajali na kufariki ni 759, abiria waliopanda pikipiki na kufariki kwa ajali wakiwa 283 huku wananchi waliokuwa wakitembea kwa miguu na kugongwa na pikipiki wakiwa 71.

“Nitoe wito kwa madereva wote wanaoendesha pikipiki kuzingatia sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoathiri wananchi wengi na kupunguza nguvu kazi katika taifa letu,” amesema.

Aidha, Naibu Waziri Sillo ametoa wito kwa wananchi kuepuka kupanda pikipiki zaidi ya mtu mmoja maarufu kama ‘mishikaki’ ili kuepuka madhara makubwa zaidi.

Send this to a friend