Serikali: Tumebakisha maombi 30,000 kati ya 120,000 kuungansha umeme nchi nzima

0
27

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, Waziri wa Nishati, January Makamba amewahahakikishia wananchi wa Sengerema kuwa maombi yao ya kuunganishiwa umeme ifikapo Agosti yatakuwa yamefanyiwa kazi.

Akijibu swali la Mbunge wa Sengerema, Khamis Tabasamu kuhusu wateja walioomba umeme miaka michache iliyopita na hawajaunganishiwa, Waziri Makamba amesema hakuna maombi yatakayoachwa kufanyiwa kazi na TANESCO kwa sababu kwa sasa (TANESCO) haina changamoto yoyote ya mita, nguzo wala nyaya.

“Mwezi wa tisa mwaka jana wakati naingia wizarani kulikuwa na maombi 120,000 tukaweka mikakati thabiti kwa pamoja na sasa yamebaki maombi 30,000 tu na hii ni ndani ya miezi 10 nikiwa wizarani,” amesema.

Uber yashtakiwa na wanawake 550 kwa unyanyasaji wa kingono

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Said Msemo amewaambia wananchi wa Wilaya ya Sengerema kuwa, ifikapo Agosti maombi yote yaliyoombwa kabla ya Juni 5 mwaka huu yatakuwa yamefanyiwa kazi, na hakutakuwa na maombi yatakayokuwa hayajakamilika.

Send this to a friend