Serikali: Wananchi puuzeni uzushi wa madai ya kumpa sumu Tundu Lissu

0
166

Serikali imekanusha tuhuma zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikiihusisha na kinachodaiwa kuwa ni kuwepo mpango wa kumwekea sumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa imewaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote.

“Serikali haijawahi kuwa na mpango wa kumwekea sumu mtu yeyote aliyepo gerezani wala haina mpango wa kufanya hivyo kwa mtu yeyote, ” imesema taarifa hiyo.

Aidha, imesisitiza kuwa taarifa hizo zimechapishwa kwa nia ovu ya kuchafua sifa na heshima kubwa ya Tanzania na tayari mamlaka zimeanza kuchukua hatua dhidi ya waliohusika kuchapisha na kusambaza uongo huo.

Send this to a friend