Serikali: Watanzania wamechoka kuona Taifa Stars ikifungwa kila siku

0
38

Serikali imesema imeandaa mpango wa kusaka vipaji vya Watanzania kwenye maeneo yote ya nchi vitakavyoleta mabadiliko katika timu ya taifa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa alipokuwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa na kusema kuwa, Serikali haitosita kuwaweka pembeni wachezaji wenye majina makubwa ikiwa hawezi kulitumikia taifa.

Ufafanuzi wa TFF  kuhusu usajili wachezaji wa kigeni

“Wale wenye majina makubwa hawalitumikii taifa hili, hawataki kulitumikia taifa hili, hawaweki uzalendo, wamekuwa na mambo ambayo sisi kama Wizara tunashindwa kuyaelewa”amesema.

Aidha, Mchengerwa amesema Watanzania wamechoka kuona timu yao ikifungwa kila siku na timu za kawaida, hivyo wanataka kuona mabadiliko makubwa katika Sekta ya michezo na Serikali inakwenda kufanya mabadiliko hayo.

Send this to a friend