Serikali: Watu 60,000 wanaambukizwa VVU kila mwaka

0
10

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kiwango cha maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi ni watu 60,000 kila mwaka, ambapo vijana wanaopata maambukizi ni takribani asilimia 34.3 ya maambukizi mapya.

Akisoma hotuba ya ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 bungeni jijini Dodoma, Majaliwa amesema watu 1,536,842 kati ya watu 1,690,948 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi.

Utafiti: Masalia ya ARV yabainika kwenye nyama ya kuku na nguruwe

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema WAVIU 1,545,880 wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU, ambapo watu wazima wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ni asilimia 96.4.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa UKIMWI bado ni tishio kama takwimu zinavyoonesha.

Send this to a friend