Serikali ya ACT Wazalendo kurejesha mradi wa Bandari ya Bagamoyo

0
43

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kikishika dola baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kitarejesha miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao umesimama.

Hayo yamesemwa na mwanachama mpya wa chama hicho, Bernard Membe wakati akipokelewa rasmi ndani ya chama hicho akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM) alikofukuzwa.

Amesema kuwa mradi huo ungewezesha kukuza uchumi kwa sababu meli kubwa zaidi zingeweza kuja nchini, ambazo pia zingelipiwa na wananchi wengi zaidi wagepata ajira.

Mbali na hilo amesema kuwa serikali ya ACT Wazalendo itashughulikia mradi wa gesi Mtwara ili uwanufaishe wananchi moja kwa moja, pamoja na kuhakikisha uwepo wa masoko imara ya mazao ya biashara.

Send this to a friend