Serikali ya Kenya yaendelea kumpambania binti aliyehukumiwa kifo Vietnam

0
7

Serikali ya Kenya inafanya juhudi za haraka kuzuia kunyongwa kwa Margaret Nduta (37), Mkenya aliyekamatwa nchini Vietnam miaka miwili iliyopita na kuhukumiwa kifo kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt. Korir Sing’Oei, amesema serikali inajitahidi kufanya kila linalowezekana na tayari imewasiliana na maafisa wa Vietnam akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Nguyen Minh Hang, kuhusu suala hilo.

Seneta wa Kisii, Richard Onyonka, amemwomba Rais William Ruto aingilie kati kidiplomasia ili kuokoa maisha ya Nduta huku akitaka serikali iombe msamaha kwa Vietnam na kuhakikisha adhabu ya kifo inabadilishwa kuwa kifungo cha maisha au adhabu nyingine mbadala.

Margaret ambaye anatarajia kunyongwa usiku wa leo, ameeleza kuwa alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya aina ya Cocaine kilogram mbili.

Send this to a friend