Serikali ya Uganda imetoa agizo kwa watoa huduma za mtandao kuzuia tovuti za ponografia ili kuwalinda vijana wa taifa hilo kutokana na athari zinazotokana na maudhui hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Thomas Tayebwa kuagiza Serikali kuzuia maudhui yote ya ngono ili kuwalinda vijana wasio na hatia dhidi ya walaghai wa mitandaoni na machapisho ya mitandao ya kijamii yasiyofaa.
“Vijana wetu wanaoneshwa ponografia. Katika nchi za Kiislamu, ponografia imezuiwa. Niambie ni kiasi gani tunaweza kupoteza kama uchumi ikiwa tutazuia tovuti za ponografia nchini. Ponografia inatuua,” amesema Tayebwa.
Utafiti: Mtindo wa kujamiiana unaoweza kuvunja uume
Mnamo mwaka wa 2017, Serikali ya Uganda iliunda kamati ya kudhibiti ponografia iliyopewa jukumu la kugundua na kupiga marufuku picha za ponografia ndani ya mipaka ya nchi.
Kamati hii iliweza kufikia hata kutumia Ksh.12 milioni [TZS milioni 208] kupata mashine maalum ambayo inaweza kugundua maudhui yote ya ponografia nchini Uganda.