Serikali yaagiza kuchukuliwa hatua wafanyabiashara ambao hawajaboresha mashine za EFD

0
43

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Dkt Edwin Mhede amesema mamlaka hiyo haitaongezi muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD badala yake itachukua hatua za kisheria kwa ambao bado hawajaboresha.

Akifungua mkutano mkuu wa nusu mwaka wa mamlaka hiyo amesema jambo la kuongeza muda haliwezekani kwani zoezi hilo linaweza kufanyika kwa muda mfupi na walipewa muda wa kutosha kuanzia Desemba 7, 2020 hadi Januari 7,2021.

“Suala la EFD mashine zenye protocol 2.1 sio chagua la mfanyabiashara bali ni lazima kila mfanyabiashara awe amefanya maboresho haya maboresho ni lazima yaendane na aina ya mashine tunazozitumia hivi sasa na upatikanaji wake ni wa dakika chache kwahiyo nasema kuongeza muda ni jambo ambalo haliwezekani inajulikana wazi kuwa utiifu wakati mwingine lazima watu walazimishwe,” amesema Dkt Mhede.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa TRA, Msafiri Mbibo amesema kuwa mkutano huo utasaidia kuweza kujua namna ya kutatua matatizo yaliopo katika sekta yao pamoja na kupanua mikakati itakayo saidia kupata mapato mengi yatakayo wezesha kufikia malengo waliojiwekea.

Send this to a friend