Serikali yaahidi kuifanyia marekebisho Sheria ya Huduma za Habari

0
37

Waziri wa Habari, Utamadani, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe  ameahidi kuwa baadhi ya vifungu vya sheria inayoongoza maudhui katika vyombo vya habari vitafanyawa mabadiliko kutokana na vifunu hivyo kuwa changamoto.

Akizungumza katika kikao maalum baina yake watayarishaji wa vipindi vya maudhui ya ndani Alhamisi (Julai 25, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya habari inapiga hatua kubwa za maendeleo na kutoa mchango unaostahiki katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mwakyembe alisema Serikali inatambua wajibu na umuhimu wa tasnia ya habari nchini, na hivyo imetunga sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza vyombo vya habari ikiwemo televisheni, ambapo vimewekwa utaratibu wa kurusha na kuandaa vipindi mbalimbali kupitia miongozo inayotolewa mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Tunatambua kuwa kuna baadhi ya vifungu vya kisheria vinavyoongoza maudhui ya vituo vya utangazaji vimekuwa changamoto, kwa kuwa Sheria hizi sio biblia au msahafu takatifu, tunaweza kuzifanyia marekebisho kila baada ya kipindi cha miaka 3-4 ili kuona ni namna gani inasaidia sekta ya utangazaji sambamba na kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza.

Aidha Waziri Mwakyembe alisema Wizara yake ipo tayari kupokea aina yoyote ya ushauri, mapendekezo na maoni ya wadau wa wazalishaji na waandaji wa vipindi vya Televisheni hususani masuala yote ambayo yamekuwa yakiwaletea changamoto katika  utekelezaji wa majukumu yao ya kuhabarisha umma kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vimekuwa daraja la kuwaunganisha Watanzania.

Dkt. Mwakyembe alisema katika mfumo uliopo sasa wa kutangaza maudhui ya ndani kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika kanuni, sheria na taratibu ambazo zimekuwa zikileta malalamiko kutoka kwa wadau, na hivyo Serikali itahakikisha kuwa vipengele hivyo vinafanyiwa kazi kwa kuwa Serikali na vyombo vya habari vyote kwa pamoja vimekusudia kujenga msingi imara wa ushirikiano baina yao.

Send this to a friend