Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini

0
6

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu itaendelea kufanya maboresho zaidi ya mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuifanya Tanzania kuendelea kuwa sehemu salama zaidi ya uwekezaji.

Ametoa kauli hiyo leo Aprili 3, 2025 wakati wa uzinduzi wa Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini (MKUMBI II) katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia mpango ambao ameuzindua, maandalizi yake pamoja na kamati zake, Serikali itaweza kushughulikia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, na kiteknolojia na kuweka mazingira bora zaidi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

“Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wadau wote ili kufanikisha malengo ya kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara. Ni mategemeo yetu kuwa, mpango huu utaongeza tija kubwa kwa Taifa letu na kusaidia kufikia malengo yetu ya kuwa na uchumi wa kati ulio endelevu,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amebainisha umuhimu wa MKUMBI II kuwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani, kuongeza fursa za ajira, kuboresha miundombinu, upatikanaji wa soko la kimataifa kwa bidhaa za ndani, kukuza ushindani na ubora wa bidhaa.

Send this to a friend