Serikali yachuguza shule inayodaiwa kufundisha wanafunzi kulawiti
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imetuma timu maalum kwenda mkoani Kilimanjaro kuchunguza tuhuma juu ya taarifa kuhusu wanafunzi kufundishwa vitendo vilivyo kinyume na maadili katika baadhi ya shule mkoani humo kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari mwanzoni mwa wiki hii.
Akizungumza leo Januari 17, 2023 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Prof. Mkenda amesema timu hiyo inayoongozwa na kamishna wa elimu, Mwanasheria wa Wizara na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora tayari imeanza uchunguzi katika shule zilizotajwa na hatua za haraka zitachukuliwa kwa wahusika wote watakaobainika kuhusika na kadhia hiyo.
Upinzani Afrika Kusini kuishitaki Serikali kutokana na kukatika umeme
“Tumeshtushwa sana na jambo hilo, tumelichukua suala hili kwa umuhimu mkubwa tumeongea na mkuu wa mkoa na kama kuna jinai yeyote basi hatua za kisheria zichukuliwa mara moja,” amesema.
Waziri Mkenda ameongeza kuwa wizara ya elimu itatoa namba maalumu ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo hivyo ambavyo vinavyochafua taswira ya elimu pamoja na kuondoa imani ya wazazi kwa shule hizo.
“Katibu Mkuu atatangaza namba ambayo mtu yeyote akijua kuna vitendo kama hivyo kwenye shule au chuo chote nasi tutaifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi ili kudhibiti vitendo hivyo” ameeleza Prof. Mkenda.